Wednesday, November 9, 2011

Picha ya Wadau wa Networking kutoka sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi katika mkutano uliofunguliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Peter Kayanza Pinda. Marchi 11 2008 Blue Pearl Hotel -Dar-es-salaam


Mtandao wa Asasi za Kijamii Tanzania na kwingineko? Mtandao wa Asasi za kijamii Tanzania (Tanzania Community Foundations Networking) ni muungano wa asasi za jamii nne ambazo ziko hapa Tanzania.Kuna

  1. Kinondoni (Kinondoni Municipal Community Foundation),
  2. Morogoro (Morogoro Municipal Community Foundation),
  3. Mwanza  (Mwanza Municipal Community Foundation)  
  4. Arusha    (Arusha Municipal Community Foundation). 
Mtandao huu ulianzishwa mnamo mwaka 2009 kwa madhumuni ya Kushirikiana katika kupeana habari na kubadilishana uzoefu. Kushirikiana katika kuanzisha miradi ya pamoja kama kuwa na mafunzo ya aina moja. Kubuni mbinu mbalimbali za kuongoza asasi hizi kwa njia ya uwazi na uaminifu kwa madhumuni ya kupata mafanikio endelevu.

Mtandao huu utaishauri Serikali kuweka mazingira mazuri ili asasi za Maendeleo ya jamii ziweze kufanya kazi katika maeneo mbalimbali hasa kutazama mfumo wa kodi uliopo kama unahitaji kufanyiwa marekebisho au kuongezewa vifungu. Asasi za kijamii zimeungana na kuunda jumuiya ya Afrika Mashariki ya utoaji misaada (East Africa Association of Grantmakers) ambayo makao yake yapo Nairobi, Kenya.

Asasi hizi zina uhusiano na Muungano wa asasi za kijamii ulimwenguni(Global Fund for Community Foundations) ambayo makao yake yapo Ubelgiji. Global Fund for Community Foundations inatoa msaada kwa asasi za jamii zinazoanza kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kuwalipia sehemu za gharama za uendeshaji na kutoa mafunzo kwa wajumbe wa Bodi na watendaji. Hadi sasa Global Fund for Community Foundations imetoa msaada kwa AMCF wa Kulipia Mjumbe wa Bodi Bibi Chiku Issa kuhudhuria Mkutano wa Community Foundations Liverpool UK. Mwaka 2009 imelipia gharama za kusafiri na malazi kwa wajumbe wawili wa AMCF Dr E.C.Njau- Mwenyekiti na mratibu E.S.Mkonyi kwa safari ya mafunzo kwa vitendo huko Afrika ya Kusini. Global Fund haikuishia hapo mwaka huu 2010 imeendelea kutoa msaada wa shilingi milioni 9.6 kwaajili ya kuanzisha mfuko wa Ruzuku ya kulipia wanafunzi gharama za Elimu kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu na nyingine za kulipia gharama za uendeshaji wa shughuli za AMCF.

Kutokana na mtandao huu wa Global Fund tumepata marafi ki kutoka Jamhuri ya Slovakia na Afrika Kusini nao ni: Healthy City Community Foundation ya Bariska Bystrica ya Slovakia. Centre for Philanthropy Bratislava ya Slovakia. Greater Rustenburg Community Foundation ya Afrika ya Kusini. 

No comments:

Post a Comment